MFANYABIASHARA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHUHUDIA LIVE VIBANDA VYAKE VIKITEKETEA KWA MOTO SOKO LA SAMUNGE

Na Ahmed Mahmoud - Arusha
Mfanyabiashara aitwaye James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono  amefariki dunia baada ya kufika na kushuhudia vibanda/maduka yake yote yakiwa yameteketea na moto kutokana na moto mkubwa kuzuka na kuunguza soko la Samunge jijini Arusha.

Akiongea na waandishi wa habari Sokoni hapo Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Koka Moita amesema tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa 23:30  katika soko la Samunge, lililopo Mtaa wa NMC, kata ya Kati, Tarafa ya Themi, katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Amesema chanzo cha moto huo uliowaka na kuteketeza vibanda vya Soko hilo hakijajulikana na idadi na mpaka sasa thamani ya mali zilizoteketea haijajulikana.

"Wakati zoezi la kuzima moto likiendelea mtu mmoja aliyefahamika kwa majina ya James Peter Temba, 57 Mfanyabiashara na mkazi wa Moshono ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa vibanda vilivyoungua ndani ya Soko hilo, alifika eneo hilo na kukuta vibanda vyake vimeteketea kwa moto alipata mshtuko na kuanguka chini na kuzimia ambapo alichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru na alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu",ameeleza Kamanda.. 

Ameeleza kuwa vibanda hivyo vilikuwa vinamilikiwa na wafanyabiashara wa Soko hilo ambavyo vilijengwa kwa Mabati, Mbao na Mabanzi. Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Wananchi walifanikiwa kuzima moto huo ambao haukuleta madhara kwa binadamu vimeungua.

Hata hivyo Uchunguzi unaendelea ili kubaini thamani halisi ya mali zilizoungua pamoja na chanzo cha moto huo. 

Soko la Samunge likiteketea kwa Moto kama lilivyokutwa na kamare ya matukio jijini Arusha usiku wa kuamkia leo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Soko la Samunge likiteketea na Moto usiku wa kuamkia leo jijini Arusha ambapo imeelezwa kuwa thamani ya Mali iliyoteketea bado haijajulikana huku mfanyabiashara Mmoja akifariki kwa mshtuko Mara baada ya kukuta maduka yake matatu yameungua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527