UZINDUZI WA MRADI WA ''VUKA INITIATIVE '' NA KAMPENI YA ''MWOGESHE MWANAO'' WAFANA ARUSHA

 Mkurugenzi wa Bushback Safari Mustapha Panju akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Mradi wa ''Vuka Initiative'' pamoja na kammpeni ya Mwogeshe Mwanao iliyofanyika katika Hoteli ya Corrido Spring iliyopo Jijini Arusha

Mwanzilishi wa wa ''Vuka Intitiative'' bi Veronica  Ignatus akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya ''Mwogeshe Mwanao''

 Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Afrika Daniel Urio akizungumza katika uzimduzi wa mradi wa ''Vuka Initiative'' sambamba na Uzindizi wa kampeni ya Muogeshe mwanao
Veila Wilson Mwalimu wa shule ya msingi Meru mkoani Arusha ambapo ni Mwalimu wa lugha ya Alama akizungumza katika uziinduzi wa kampeni ya ''Mwogeshe Mwanao''
Mkurugenzi wa Bushback Safari Mustapha Panju akizungumza katika uzinduzi rasmi wa Mradi wa ''Vuka Initiative'' pamoja na kammpeni ya Mwogeshe Mwanao iliyofanyika katika Hoteli ya Corrido Spring iliyopo Jijini Arusha
Mtayarishaji wa Keki Elizabeth Membe akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye keki hapa (hayaonekeni)
Mwanzilishi wa Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus akikata keki na mmoja wa wageni Rasmi Mrs Mustafa Panju ishara ya uzinduzi rasmi wa Kampeni ya ''Mwogeshe Mwanao'' iliyofanyika Jijini Arusha katika Hoteli ya Corrido Spring
Keki iliyotumika katika Uzinduzi wa Kampeni ya ''Mwogeshe Mwanao''



Mwanzilishi wa Vuka Initiative bi Veronica Ignatus akimlisha keki mwanamke mwenye umri mkubwa (Mama Lily)aliyehudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya Mwogeshe mwanao iliyofanyika Jijini Arusha ikiwa pia ni maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Mwanzilishi wa Vuka Initiative bi Veronica Ignatus akimlisha keki msichana mwenye umri mdogo aliyehudhuria katika uzinduzi wa kampeni ya Mwogeshe mwanao iliyofanyika Jijini Arusha ikiwa pia ni Maadhimisho ya siku ya  wanawake duniani.



Shamrashamara zikiendelea katika uzinduzi wa Kampeni ya Mwogeshe Mwanao katika ukumbi wa Corrido Spring Hotel iliyopo Jijini Arusha



Shughuli zikiendelea ukumbini kama inavyoonekana
Mwanzilishi wa ''Vuka Initiative'' Bi Veronica Ignatus  akiwa na baadhi ya wanawake mara baada ya kufanyika kwa Uzinduzi wa kampeni ya'' Mwogeshe Mwanao'' iliyofanyika katika hotel ya Corrido Spring Hotel Jijini Arusha

 Mwanzilishi wa  Mradi ''Vuka Initiative''  bi Veronica Ignatus akiwa kayika picha ya pamoja ba baadhi ya viongozi na wageni waalikwa katika uzinduzi wa Kampeni ya ''Mwogeshe Mwanao'' 


Na Mwandishi wetu, Arusha.

Katika kusheherekea sikukuu ya wanawake duniani Machi 8,2020 wazazi na walezi wametakiwa kujenga uhusiano wa karibu na Watoto wao na kutenga muda malezi na ufuatiliaji wa karibu mabadiliko ya tabia za watoto.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Bushbuck Safari Mustapha Panju alipokuwa akizindua mradi wa “Vuka Initiative” pamoja na uzinduzi wa kampeni ya  Mwogeshe Mwanao iliyofanyika katika Hoteli ya Corrido Spring mkoani Arusha.

Mustapha Panju ameitaka jamii kubadilika kifikra na kuacha visingizio vya kubanwa na  majukumu ya kila siku kwa kisingizio cha kupanda kwa haki ya maisha badala yake watenge muda wa kuwa na watoto wao mara kwa mara kwani watoto wengi wamewazowea wasaidizi wa majumbani kuliko wazazi wao au walezi wao halisi


Mwanzilishi wa Mradi wa Vuka Initiative Bi Veronica Ignatus
alisema kuwa Vuka Initiative” ni mradi wenye kusudi la kupunguza changamoto za ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii. Dira yake ni kuwa taasisi kimbilio kwa watu wote wenye changamoto za kimaisha.




Pia alisema kuwa Dhima yake ni kuifikia jamii na kutatua changamoto za ukaliti na unyanyasaji wa kijinsia ambapo Motto
wao unaowaongoza ni “Vuka yako, Salama yako”

Bi Veronica alisema kuwa mradi huu unatarajia kuanza kufikia watoto na wanawake katika makundi ya wanawake yaani wafanyakazi wa sekta rasmi na zisizo rasmi, mpango ni kuanzia na wilaya sita za mkoa wa Arusha.

Vuka Initiative umelenga kwa dhati kuisaidia serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli ya kuwaboreshea maisha na kuwawezesha wanawake na watoto.

Namna au mbinu ya kuifikia jamii itakuwa kwa kuandaa vipindi, warsha, semina, makongamano ya kuwafikia wanawake na Watoto.


Vuka Initiative itatumia kampeni ya “Mwogeshe Mwanao” kampeni hii inalenga kuwakumbusha wazazi na jamii kwa
ujumla kuhusu jukumu la kuongeza ukaribu/mahusiano kwa watoto wao na kutenga muda wa malezi na ufuatiliaji wa karibu kwa Watoto wetu.


Vuka Initiative inatoa wito kwa jamii, vyombo vya habari na wadau mbalimbali kuunga mkono kwenye tukio na kuwa huru
wakati wote kutoa ushauri, mapendekezo, maoni na michango ya hali na mali katika kuwezesha utekelezaji wa majukumu ya kuitumikia jamii na Taifa kwa ujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527