MENEJA WA DIAMOND 'SALAM SK' APATA CORONA....JOKATE, WASANII MBALIMBALI WAMPA POLE


Meneja wa mwanamuziki nyota nchini Diamond Platnumz,   aitwaye Sallam SK,    ametangaza kuambukizwa virusi vya Corona,  lakini amewatoa hofu Watanzania na kuwa anaendelea vizuri.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sallam amepost picha na kuandika caption hii;

HABARI…!! Napenda kuwajulisha na kuwatoa hofu ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na Corona Virus, kwa sasa nipo chini ya uangalizi mzuri na afya yangu inaendelea vizuri.

Pia naishukuru serikali kwa maandalizi mazuri na huduma ninayopata wodini, kwenye kituo toka juzi nipo peke yangu kama nimekikodisha vile 😅, wahudumu wana ushirikiano mzuri Mungu awalinde na awape afya njema maana wamejitolea nafasi zao kutupatia huduma sisi waathirika.

Hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye wizara husika, naomba kwa wote tuwe salama na familia zetu, tuchukue tahadhari mapema. Be Strong and Be Safe Everyone out there #AllahBlessUsAll.

Baadhi ya wasanii na watu mashuhuri  waliompa pole ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo, msanii Ambwene Yesaya ‘AY’, Rita Paulsen, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Hamisi Taletale ‘babutale’, Mbwana Yusuph ‘Mbosso’ na wengine wengi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527