MAGARI YAANZA KUPITA KATIKA DARAJA LA KIYEGEYA – MOROGORO – DODOMA…TAZAMA PICHA HAPA
Ujenzi wa Daraja la Kiyegeya lililopo katika barabara ya Morogoro – Dodoma unaendelea ambapo  magari yaliyokuwa yamekwama katika eneo hilo yameanza kuruhusiwa kupita.

Malunde 1 blog iliyopita katika eneo hilo leo Alhamis Machi 5,2020 majira ya saa tano asubuhi hadi saa saba mchana leo imeshuhudia magari yakiwemo mabasi yanayotoka Jijini Dar es salaam kuelekea Dodoma, Shinyanga na Mwanza na yanayotokea Dodoma kuelekea Morogoro yakipita katika daraja hilo ambalo lilikatika baada ya kusombwa na maji majira ya saa tisa alasiri Machi 2,2020.

Licha ya msururu mrefu wa magari hususani malori ya mizigo,Malunde 1 blog imeshuhudia askari wa Kikosi cha Usalama barabarani wakiongoza magari yakiwemo mabasi kupita katika daraja hilo.

Jana Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alikagua kazi ya ukarabati wa daraja la Kiyegeya ambalo baada ya kukatika kwa kusombwa na maji limesababisha mawasiliano kati ya Morogoro na Dodoma kukatika.

Aliwataka wananchi na wasafiri kuwa wavumilivu wakati huu ambapo utengenezwaji wa daraja hilo lililokatika unaendelea. 

Aidha Waziri Mkuu,alimuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi pamoja na wakandarasi wa mkoa wa Dodoma na Morogoro kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuwezesha ujenzi wa daraja hilo kumalizika haraka. 

"Naagiza Jeshi la Wananchi Tanzania pamoja na wakandarasi wote wa Dodoma na Morogoro kuja hapa na kufanya kazi usiku na mchana ili hadi kesho barabara ianze kupitisha magari hata madogo na itafutwe njia mbadala kwa ajili ya magari makubwa kupita",amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

ANGALIA PICHA LEO KATIKA DARAJA LA KIYEGEYA
Muonekano wa daraja la Kiyegeya linalounganisha Morogoro na Dodoma leo Machi 5,2020 ambapo magari yameruhusiwa kuanza kupita. Picha zote na Kadama Malunde -Malunde 1 blog
Muonekano wa daraja la Kiyegeya linalounganisha Morogoro na Dodoma leo Machi 5,2020. Sehemu hiyo ndipo magari yanapita moja baada ya jingine.

Muonekano wa daraja la Kiyegeya linalounganisha Morogoro na Dodoma leo Machi 5,2020.

Msururu wa Magari yanayotokea mkoani Morogoro kuelekea Dodoma kabla ya kulifikia daraja la Kiyegeya linalounganisha Morogoro na Dodoma leo Machi 5,2020.

Msururu wa Magari yanayotokea mkoani Dodoma kuelekea Morogoro kabla ya kulifikia daraja la Kiyegeya linalounganisha Morogoro na Dodoma leo Machi 5,2020.
Lori baada ya kupita katika daraja la Kiyegeya likitoa Dodoma leo Machi 5,2020.
Msururu wa Magari yanayotokea mkoani Dodoma kuelekea Morogoro kabla ya kulifikia daraja la Kiyegeya linalounganisha Morogoro na Dodoma leo Machi 5,2020.

Msururu wa Magari yanayotokea mkoani Dodoma kuelekea Morogoro kabla ya kulifikia daraja la Kiyegeya linalounganisha Morogoro na Dodoma leo Machi 5,2020.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post