SHUWASA YATOA UFAFANUZI MABOMBA YA MAJI KUPASUKA SHINYANGA


Kushoto ni Mkurugenzi wa SHUWASA  Flaviana Kifizi akiangalia bomba la maji lililopasuka katika  eneo la  Kata ya Masekelo jirani na Mto Kidalu leo Jumatatu Machi 16,2020. 


Na Marco Maduhu  - Shinyanga
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA),imetolea ufafanuzi kukithiri kwa upasukaji wa mabomba ya maji kuwa tatizo ni kubwa ni wananchi kupunguza matumizi ya maji hasa kipindi hiki cha Mvua hali inayosababisha  mgandamizo mkubwa wa maji na hatimaye bomba kupasuka.

Hayo yamebainishwa leo Jumatatu Machi 16,2020 na Mkurugenzi wa SHUWASA Bi. Flaviana Kifizi, wakati akizungumza na waandishi wa habari eneo la  Kata ya Masekelo jirani na Mto Kidalu  ambapo matengenezo ya bomba la mm 600 yakiendelea.

“Napenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na  tatizo la upasukaji wa mabomba ya maji  kutokea mara kwa mara na baadhi ya wananchi wakilalamika  kukosekana kwa huduma ya maji  hasa maeneo ya viwanda, vyuo, mashuleni,sababu kubwa ni ndio hiyo mabomba yanazidiwa kutunza maji ndiyo maana yanapasuka”,alisema Kifizi.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa wananchi wa Shinyanga kutoa taarifa za uvujaji pindi wanapoona upasukaji wa mabomba ili kushughulikiwa kwa haraka.
Aliendelea kwa kusema tarehe 16 Machi ni Maadhimisho ya Wiki ya Maji Dunia na wito kwa wateja wenye madeni ya muda mrefu kufika ofisini na kulipa deni kwa awamu na kurudishiwa huduma bila faini yoyote na Ofa hii hadi Machi 30 mwaka huu.

Pia alisema ujenzi wa mradi wa maji katika Kata ya Mwawaza, wenye gharama ya Shilingi Bilioni 1.5 ambao ulianza Januari mwaka huu  hadi kufikia mwezi Aprili utakuwa umeshakamilika kujengwa, na kuanza kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Kata ya Mwawaza na Mamlaka inaendelea kuongeza huduma ya maji kwa awamu kwa Maeneo yasiyokuwa na mtandao wa maji.
Mkurugenzi wa SHUWASA Bi. Flaviana Kifizi (mbele) akiwa na Afisa Uhusiano na umma wa SHUWASA Bi. Nsianel Gelard (nyuma) wakivuka mto Kidaulu wakielekea eneo la Masekelo kuangalia bomba la maji lililopasuka na kufanyiwa matengenezo na mafundi wa SHUWASA leo Jumatatu Machi 16,2020 . Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog
Kushoto ni Mkurugenzi wa SHUWASA Bi. Flaviana Kifizi akiangalia bomba la maji lililopasuka  katika eneo la  Kata ya Masekelo jirani na Mto Kidalu leo Jumatatu Machi 16,2020. 
Kushoto ni Mkurugenzi wa SHUWASA Bi. Flaviana Kifizi akizungumza na waandishi wa habari katika  eneo la  Kata ya Masekelo jirani na Mto Kidalu ambapo bomba la maji limepasuka.
Mafundi wa SHUWASA wakitoa maji ili watengeneze bomba la maji lililopasuka.
Picha zote na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527