MWANAMKE AJIUA KARANTINI YA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, March 28, 2020

MWANAMKE AJIUA KARANTINI YA CORONA

  Malunde       Saturday, March 28, 2020

Sehemu ya Shule ambayo imetengwa maalum, kwa watu wanaoingia Kenya kutoka nchi zilizoathiriwa na Virusi vya Corona.

Mwanamke mmoja raia wa Afrika kusini amejitia kitanzi kwenye karantini ya Shule ya Ufundi nchini Kenya (KITI), iliyopo Mjini Nakuru, eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya watu wanaoingia nchini humo kutoka Mataifa yaliyoripotiwa kuwa na ugonjwa wa Virusi vya Corona.

Jeshi la Polisi nchini humo kupitia kwa Kamishna wa Nakuru George Natembeya, amethibitisha kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, alijitoa uhai kwa kujinyonga na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha hatua hiyo.

Akizungumzia tukio hilo Waziri wa Afya kaunti ya Nakuru Dkt Kariuki Gichuki, amesema mwanamke huyo aliingia nchini Kenya Machi 25 mwaka huu na alitakiwa kusalia eneo hilo kwa siku 14, kabla ya kukutwa chumbani kwake akiwa amefariki dunia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post