KAULI YA DPP KUHUSU SAKATA LA KANGI LUGOLA NA WENZAKE | MALUNDE 1 BLOG

Friday, March 13, 2020

KAULI YA DPP KUHUSU SAKATA LA KANGI LUGOLA NA WENZAKE

  Malunde       Friday, March 13, 2020

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga, amesema bado ofisi yake na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), wanalifanyia kazi sakata la tuhuma za aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na aliyekuwa Kamishna wa Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.

Alisema taasisi hizo mbili zina utaratibu wa kufanyakazi na kwamba hakuna jambo la kificho, kila kitu kitakapokuwa tayari umma utafahamishwa kupitia vyombo vya habari.

Akizungumza na waandishi habari ofisini kwake  alisema kuna utaratibu wa utendaji wa kazi zao hivyo suala hilo likiiva litawekwa hadharani.

"Kwa sasa sina majibu siwezi kusema jalada la Kangi na Andengenye kama limefika ofisini kwangu au la, sina utaratibu wa kutoa taarifa nusu nusu, muda ukifika nitawaita niwaeleze kinachoendelea," alisema DPP.

Lugola alivuliwa madaraka baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kusikitishwa na utendaji wa viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani hasa utiaji saini wa mkataba wa mradi wa thamani ya Euro milioni 408.

Aliamua kutengua uteuzi wa Lugola wa Uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene na kisha kuagiza TAKUKURU Wamchunguze na wachukue hatua.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post