HALIMA MDEE AMWAGA MACHOZI BAADA YA KUTOKA GEREZANI...."WATANZANIA HAMJUI NI JINSI GANI MLIVYOTULIZA, HATUKUTEGEMEA "


Mbunge Halima Mdee amemwaga machozi hadharani baada ya kutoka gereza la Segerea leo na kuwashukuru watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha wa kuwachangia na kuwafanyaa wao kuwa nje ya gereza.



"Watanzania nyie hamjui, hamjui mlivyotusitiri mimi ni kamanda lakini napata hisia nilikua najua tulivyonyong'onyezwa watu walivyo na aibu mbaya watakuwa wamekata tamaa ila wametuchangia tunashukuru na bado pesa zinaingia mimi nalia sio kwamba naogopa hapana ila upendo wenu muliouonyesha kwetu" alisema huku akiwa analia Halima Mdee.

Wabunge Halima Mdee, Esther Matiko na Ester Bulaya wametoka gereza la Segerea leo baada ya kulipa faini ya Sh110 milioni.

==>>Tazama hapo chini
Video Credit:EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527