GODBLESS LEMA ADAI KUITWA POLISI ARUSHA

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema amepata taarifa za kutakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi Arusha. 


Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Lema amesema kuwa kwa nyakati tofauti polisi wamefika nyumbani kwake kumtafuta.

"Nimepata taarifa kuwa gari mbili za Polisi zikiwa na askari kanzu zimekwenda kunitafuta nyumbani kwangu bila taarifa,wamenikuta nimeondoka,hivyo nimepigiwa simu na kutakiwa ofisi ya RCO Arusha.Hawajataka kusema wana nitafutia nini?nina wasiliana na Wakili wangu kuelekea."-Ameandika Lema.


Tunaendelea kufuatilia kwa kina
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post