Breaking : DEREVA WA BASI LA ISAMILO AFARIKI DUNIA AKIENDELEA NA SAFARI KWENYE BASI



Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Dereva wa Basi la Isamilo lenye namba za usajili T609 CQB Scania linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Mbeya Sebastian Mathias (43) mkazi wa Mwanza amefariki dunia wakati akiendelea na safari kutoka Mbeya kwenda Mwanza.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Machi 20,2020 majira ya saa nne asubuhi.

"Sebastian alitoka Mwanza kwenda Mbeya akiwa anajisikia vibaya. Huwa wapo madereva wawili,vwameenda hadi Mbeya,wakati wanatoka Mbeya kwenda Mwanza Sebastian alikuwa anaendelea kujisikia vibaya, walipofika Singida akawa anajisikia vibaya zaidi ndipo akabadilishana na yule dereva mwenzake",amesema Kamanda Magiligimba.

"Wamefika Tinde leo saa nne asubuhi akawa amezidiwa sana, wakambeba kwenda kwenye Kituo cha Afya Tinde,baada ya kumfikisha,Daktari akabaini kuwa tayari Sebastian Mathias alikuwa amefariki dunia",ameeleza Kamanda Magiligimba.

Amesema kwa kuwa gari hilo lina madereva wawili hivyo dereva mwingine ameendelea na safari kwenda Mwanza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527