WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 12 TANZANIA..RAIS MAGUFULI AAGIZA WASAFIRI KUWEKWA KARANTINI KWA GHARAMA ZAO


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli amesema watu 12 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini Tanzania.


Katika hotuba yake kwa Taifa kiongozi mkuu huyo wa nchi leo Jumapili Machi 22, 2020 amebainisha kuwa kuanzia kesho Jumatatu Machi 23,2020 wasafiri watakaoingia Tanzania kutoka nchi zenye maambukizi ya corona watawekwa katika eneo maalum kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.

“Mpaka sasa nchi yetu imebaini wagonjwa 12 ambao wamethibitika kuambukizwa corona. Kati yao wanne ni raia wa nje na wanane ni raia wa Tanzania. Wagonjwa wote isipokuwa mmoja ametoka kwenye nchi zilizokuwa na maambukizi ya ugonjwa huo.”

“Kuanzia kesho Machi 23 wasafiri wote watakaoingia nchini kutoka kwenye mataifa yaliyoathirika zaidi na ugonjwa huu watalazimika kufikia sehemu zilizotengwa na kukaa huko kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe”,amesema Rais Magufuli.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527