Breaking : IDADI YA WAGONJWA WA CORONA TANZANIA YAFIKIA 19
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema wagonjwa wa corona nchini Tanzania wamefikia 19 baada ya watano kuongezeka. 
Taarifa iliyotolewa na Waziri huyo leo Jumatatu Machi 30, 2020 inaeleza kuwa wagonjwa hao watano walifanyiwa vipimo katika maabara kuu ya Taifa.

“Kati ya wagonjwa hawa, watatu ni kutoka Dar es Salaam na wawili kutoka Zanzibar . Hivyo sasa jumla ya wagonjwa wa corona ni 19 akiwemo mgonjwa mmoja aliyetolewa taarifa na Waziri wa Afya Zanzibar Machi 28, 2020”,amesema.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post