ALICHOKISEMA DKT VICENT MASHINJI BAADA YA CCM KUMCHOMOA GEREZANI


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleoa (CHADEMA), Dkt Vicent Mashinji, amefunguka mengi baada ya kulipiwa faini yake na Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba ameshangazwa kuona jambo hilo lilivyomalizika kwa uharaka.


Dkt Mashinji ameyabainisha hayo leo mara baada ya kuachiwa huru, baada ya jana kushindwa kulipa faini yake na kupelekwa Gereza la Segerea na kuliomba Taifa kuendelea kuboresha zaidi Magereza.

"Niwashukuru sana ndugu zangu wa CCM, miaka miwili iliyopita nilipata kuwa hapo gerezani, sasa hivi kuna improvement kidogo, naomba kama Taifa tuendelee kuboresha maeneo yote tunayowahifadhi wananchi, nilitegemea kama kule nilikotoka hili suala lingekuwa la Kitaifa, lakini nimeshangazwa kuona limefanywa tu na Mkoa, najiona niko sehemu salama zaidi" amesema Dkt Mashinji.

Dkt Mashinji pamoja na viongozi nane wa CHADEMA, kutokana na kesi yao ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili, jana Machi 10, 2020, walihukumiwa faini ama kifungo cha miezi mitano jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527