WATUMISHI WA AFYA WAASWA KUTOSHIRIKI KWENYE UHALIFU WA KUHARIBU USHAHIDI

Na Englibert Kayombo, WAMJW – Moshi Kilimanjaro.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewaasa watumishi wa afya kutoshiriki kwenye makosa ya uhalifu kwa kuharibu ushahidi wa makosa ya jinai pindi wanapofanya uchunguzi wa kitaalam.

Dkt. Ndugulile ametoa kauli hiyo alipokuwa ziarani katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) akizungumza na watumishi wa afya hospitalini hapo.

“Katika kosa ambalo hatutamsamehe mtumishi wa afya ni kushiriki katika uhalifu wa kuharibu ushahidi, hatutamvumilia mtu ambaye atashiriki kwenye makosa hayo” alisema Dkt. Ndugulile.

Alisema kuwa kesi za ukatili wa kijinsia mara nyingi huwa ni kesi za jinai huku wataalam wa afya wakipewa dhamana ya kuthibitisha ukweli wa matukio hayo na kuwataka kufuata miiko na maadili ya taaluma ya afya.

“Mtu amepata shambulio, daktari unasema kwamba huyu mtu hajashambuliwa, tumeshawahi kufanya hiyo na endapo tukithibitisha pasipo na shaka kwamba wewe mtaalam wetu umeenda kinyume na miiko na maadili ya kazi yako lazima tutakuchukulia hatua” alisisitiza Dkt. Ndugulile.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527