WATU WALIOFARIKI DUNIA KWA VIRUSI VYA CORONA WAFIKIA 425 NCHINI CHINA


Idadi ya watu waliofariki dunia kwa ugonjwa unaotokana na virusi vya Corona imefikia 425.

Kabla ya hapo viongozi wa idara ya afya nchini humo walikuwa wametangaza kuwa idadi ya wahanga wa ugonjwa huo ni 360. 

Hata hivyo ripoti iliyotolewa jana imesema kuwa jumla ya watu elfu 990 wamelazwa katika mkoa wa Hubei na kwamba 576 kati yao wana hali mbaya. 

Virusi vya Corona viliibuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka uliopita katika soko la vyakula vya baharini la mji wa Wuhan nchini China.

Hata hivyo mbali na mji huo, virusi hivyo sasa vimeenea katika nchi 18 za dunia. Hii ni katika hali ambayo mashirika mengi ya ndege likiwemo Shirika la Ndege la Qata, Air Canada, Air France, Air Seoul, American Airlines, British Airways, Lufthansa, Turkish Airlines na mengine kadhaa, yamesimamisha safari zao kuelekea China kutokana na hatari ya virusi hivyo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post