VIGOGO WENGINE 6 WA JESHI LA ZIMAMOTO WAWASILI TAKUKURU MAKAO MAKUU DODOMA KUHOJIWA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Waliokuwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji  wa makubaliano  iliyosainiwa tarehe 22,Agosti ,2019  kati ya jeshi la zimamoto na uokoaji  na kampuni ya ROM Solutions  Co.LTD leo Feb.5,2020 wamewasili ofisi za  Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa [TAKUKURU]makao makuu jijini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kashfa ya kufanya mkataba mbovu wa Trilioni Moja bila kupitishwa na  bunge.

Idadi ya  wajumbe waliofika katika ofisi hizo leo  ni sita ambapo walifika  ofisi za TAKUKURU pamoja na kompyuta mpakato [Laptop]walizopewa na kampuni ya ROM SOLUTIONS CO.LTD.

Wajumbe hao pia walikuwa wakilipwa posho za vikao USD 800   na kampuni hiyo  wakati wakiwa wanakutana katika vikao vyao  vya majadiliano.

Wajumbe hao ni pamoja na Kamishna wa zimamoto  Mbaraka Semwanza,Naibu Kamishna  wa zimamoto Fikiri Salla,Naibu Kamishna wa Zimamoto  Lusekelo Chaula’.

Wengine ni Naibu Kamishna  zimamoto Ully Mburuko,Mchumi zimamoto Boniface Kipomela  na Mchumi  wa jeshi hilo la zimamoto na uokoaji Felis Mshana.

Ikumbukwe kuwa sakata hilo  la mkataba mbovu  wa Trilioni moja limesababisha aliyekuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugola kuachishwa wadhifa huo na kuteuliwa mwingine  hivi karibu George Simbachawene.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post