MAMA SALMA KIKWETE ATOA MSAADA WA MABATI 760 LINDI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, February 26, 2020

MAMA SALMA KIKWETE ATOA MSAADA WA MABATI 760 LINDI

  Malunde       Wednesday, February 26, 2020


Mbunge wa kuteuliwa na Mhe. Rais ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Mhe. Mama Salma Kikwete  amekabidhi mabati 500 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko, mabati 200 ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Halmashauri ya Mtama na mabati 60 ujenzi wa Shule ya Sekondari kata ya Mnara mkoani Lindi.

Akizungumza leo Jumatano Februari 26, 2020 wakati wa kukabidhi mabati hayo 760 Mama Salma Kikwete alisema : "Nimetoa mabati haya kwa kuwa mpaka sasa CCM  haina Ofisi na wenzetu waathirika wa mafuriko wamepewa maeneo lakini bado wanahitaji msaada mkubwa katika kuhakikisha wanapata huduma pamoja na sehemu ya kuishi".

"Nipo tayari kusaidia waathirika wa mafuriko kwa chochote kama nilivyojitoa kuwapa mabati haya lakini nawaomba sana Watanzania kuendelea kuwasaidia waathirika waliopo Mchinga, Kilwa na maeneo mengine ambayo bado wananchi wetu hawajapa sehemu muhimu ya kuishi",amesema.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi  Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Rukia Hassan amempongeza Mh Mama Salma Kikwete kwa kutoa mabati 200 kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi katika Halmashauri ya Mtama.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post