NAIBU WAZIRI JOSEPHAT KANDEGE AFURAHISHWA NA MIRADI YA TARURA – ILEMELAk | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, February 26, 2020

NAIBU WAZIRI JOSEPHAT KANDEGE AFURAHISHWA NA MIRADI YA TARURA – ILEMELAk

  TANGA RAHA BLOG       Wednesday, February 26, 2020
Na, Geofrey A.Kazaula

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Kandege ameelezea kuridhishwa kwake na miradi ya barabara iliyotekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini Tarura katika Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Aliyasema hayo wakati wa Ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Mwanza ambapo ameeleza kuwa mafanikio yanayopatikana katika Manispaa hiyo hasa katika miradi ya barabara yanatokana na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya wataalam wa TARURA na watumishi wengine wa Manispaa kwa kufanya kazi pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.

‘‘ Wote tumeshuhudia barabara hizi zilivyo kwenye kiwango, mafanikio haya yanatokana na Umoja uliopo kwa watumishi wote wa Manispaa ya Ilemela pamoja na watumishi wa TARURA kwani wanafanya kazi kwa pamoja ili kuwaletea wananchi wetu maendeleo, kiujumla wanafanya vizuri’’Kandege.

Aidha amesisitiza kuwa miundombinu ya barabara inapokamilika ilindwe kwa nguvu zote na amewaagiza viongozi husika huhakikisha barabara hizo zinafanyiwa usafi mara kwa mara na kulinda miundombinu ya barabara hizo.

Naye Meneja wa TARURA Manispaa ya Ilemela Mhandisi Clement Kihinga amesema kuwa barabara hizo zilizotekelezwa chini ya mradi wa Tanzania Strategic Cities Project (TSP) zimekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuinua uchumi wa wananchi na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanailinda miundmbinu ya barabara ilizidumu na ziendelee kuboresha maisha yao na kurahisisha suala la usafiri na usafirishaji katika Manispaa ya Ilemela.

‘‘Serikali inatumia gharama kubwa sana kujenga barabara hizi hivyo nitoe wito kwa wananchi kuhakikisha kila mmoja wetu anashiriki kulinda miundombinu hii ya barabara ’’ amesema Mtaalam huyo.

Mmoja wa wananchi wa Kiseke A Ilemela Issa Shabani alisema awali usafiri ulikuwa changamoto sana Katika barabar yao kwani miundombinu ilikuwa mibovu sana ila baada ya baraba ya kiseke Busweru kukamilika maisha yamepanda kiuchumi

“Sasa nafanya biashara yangu ya matunda hapa Busweru, nayabeba salama na hayaharibiki kwani barabara ni nzuri na hata kipato changu kimeongezeka hivyo naishukuru sana Serikali kwa kujenga barabara hii”Alisema Shabani

Ziara ya Mhe, Kandege inaendelea Mkoani Mwanza ambapo miradi mbalibali ya maendeleo zikiwemo barabara zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA inatarajiwa kukaguliwa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post