WIZARA YABARIKI MSAFARA WA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIAKaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara Bw. Leornard Mchau akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Msafara wa wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda mkoano Latavi tarehe 24/02/2020. Picha Zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara Bw. Leornard Mchau akizungumza na wawakilishi wa msafara wa wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda mkoano Latavi tarehe 24/02/2020.
Msanii wa  Muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal Shetta akielezea namna watakavyoupamba msafara wa wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia wakati wa mamandalizi ya kuondoka kwa msafara huo leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda mkani Katavi tarehe 24/02/2020.
Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara Bw. Leornard Mchau akiagana na Msanii wa  Muziki wa kizazi kipya Nurdin Bilal Shetta mara baada ya kuzunumza na wawakilishi wa msafara wa wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia leo jijini Dodoma utakoanzia Mpanda mkoano Latavi tarehe 24/02/2020.
**


Na Mwandishi Wetu Dodoma
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii imebariki kuanza kwa Msafara wa kitaifa wa wa kijinsia wenye lengo la kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Akizungumza na wawakilishi wa Wizara, Wadau kutoka Legal Services Facility, Wildaf na wasanii wa muziki wa kizazi kipya leo jijini Dodoma Kaimu Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bw. Leonard Mchau amesema msafara huo umeandaliwa maalum kupeleka ujumbe wa kupambana na ukatili wa kijinsia kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani.

Bw. Mchau amewaasa wawakilishi hao wa Msafara huo kupeleka ujumbe huo ambao utasaidia kuendeleza mapambano ya kutokomeza vitendi vya ukatili nchini ambavyo vimekuwa vikishamiri kila siku katika jamii.

Ameongeza kuwa Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomea kwa kasi ili watoto na wanawake wanaoathirika na vitendo hivyo kuoondokana na vitendo hivyo vinavyowanyima baadhi ya haki zao msingi.

Akizungumza kwa niaba ya Wadau Mwakilishi wa Shirika la LSF Bw. Joseph Magazi ameishukuru Serikali kwa kuwashirikisha waau katika kampeni ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika mapambano hayo.

Akizungumza kwa naiaba ya Wasanii Bw. Nurdil Bilal maarufu kama ‘Shetta’ amesema watatumia sanaa yao kufikisha ujumbe kwa jamii kwani wao ni mmoja ya wanajamii na wanapaswa kushirikiana nayo kusaidia kupambana kutokomeza vitendo vya kikatili katika jamii.

Msafara huu utaanzia katika mkoa wa Katavi wilaya ya Mpanda tarehe 24/02/2020 na kuendelea hadi tarehe 05/03/2020 katika vituo vifuatavyo, Sumbawanga, Rukwa tarehe 25/02/2020 Vwawa, Songwe tarehe 26/02/2020, Mbeya Mjini tarehe 27/02/2020 Makambako, Njombe tarehe 28/02/2020 Iringa Mjini, Iringa tarehe 29/02/2020 Tabora Mjini, Tabora Mjini tarehe 01/03/2020 Shinyanga mjini tarehe 03/03/2020 Maswa Simiyu tarehe 04/03/2020.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post