MAZISHI YA MOI HUENDA KENYATTA AKASUBIRIWA BAADA YA KUKUTANA NA TRUMP


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kulia ni Rais Mstaafu Daniel Moi wakati wa uhai wake.

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Pili wa Jamhuri ya Kenya, Daniel Arap Moi, tayari umekwishapelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kinachoitwa Cha Lee, kilichopo jijini Nairobi nchini Kenya.

Rais Mstaafu wa Taifa hilo amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Februari 4, 2020, akiwa na umri wa miaka 95, katika hospitali Jijini Nairobi alikokuwa akipatiwa matibabu na kifo chake kimetangazwa na Rais Uhuru Kenyatta, akiwa safarini kuelekea nchini Marekani katika mkutano wake na Rais Donald Trump.

Kufuatia kifo hicho Rais Kenyatta ametangaza kuwa bendera nchini Kenya na katika Ubalozi wa Kenya, kupeperushwa nusu mlingoti hadi atakapozikwa, ambapo hadi sasa taarifa za mazishi bado hazijatangazwa na huenda Rais Kenyatta akasubiriwa, kwani atarejea nchini siku ya Alhamisi ya Februari 6, 2020.

Daniel Moi aliingia madarakani mwaka 1978, baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa kwanza Hayati Jomo Kenyatta, na kuapishwa kama Rais wa Pili wa Jamhuri ya Kenya na kuhudumu kwa miaka 24, ambapo mkewe Lena Moi, alifariki mwaka 2004.

Moi ameacha watoto Saba ambao ni Gideon (Seneta Baringo), Raymond (Mbunge wa Rongai ), Jeniffer Moi, June Moi, Philip Moi, John-Mark and Doris Moi. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Daniel Arap Moi, mahala pema peponi Ameen.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post