MKURUGENZI WA KAMPUNI INAYOJENGA RELI YA KISASA AHUKUMIWA KULIPA FAINI YA DOLA MILIONI 100 AMA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU


Mkurugenzi wa Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Markez inayojenga Reli ya kisasa Standard Gauge, Yetkin Genc Mehmet ((54) raia wa Uturuki amehukumiwa kulipa faini ya USD milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukiri shtaka la kushindwa kutoa tamko la fedha USD 84,850 alizokutwa akizisafirisha.

Aidha mahakama imeamuru kutaifishwa kwa fedha hizo zote kuwa mali ya serikali.

Mehmet ambaye nchini Tanzania anaishi Ilala jijini Dar es salaam amesomewa hukumu yake na Hakimu Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba baada ya kufikishwa mahakamani leo Februari 27 ma kusomewa shtaka moja la kushindwa kuzitolea taarifa fedha alizokutwa kusafiri nazo.

Mapema akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mkuu Shadrack Kimaro amedai kuwa Februari 13, mwaka huu huko katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere terminal III jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa anaondoka nchini kwenda Instabul Uturuki alikutwa na USD 84,850 ambazo hakuwa amezitolea taarifa kwa Idara ya Forodha.

Mapema akisoma maelezo ya awali kabla ya kusomewa adhabu wakili Kimaro alidai mshtakiwa Mehmet ni raia wa Uturuki na ameajiliwa na kampuni ya Yapi Merkezi  ambayo inashughulika na ujenzi wa reli ya kisasa Standard Gauge hapa nchini Tanzania.

Imedaiwa siku hiyo alikuwa akisafiri kuelekea Instabul Uturuki kwa kutumia ndege ya Turkish namba TK 0604 huku akiwa amebeba mabegi. Akiwa amefuata taratibu zote za uwanja wa ndege akiwa anaelekea kupanda ndege alikutwa na Ofisa wa usalama akiwa na kiasi hicho cha fedha ambazo hakuwa amezitolea taarifa.

Aidha imedaiwa fedha hizo zimehifadhiwa NMB banki kwenye kitendo cha intelejensia.

Mahakama pia imeamuru mshtakiwa kurudishiwa pasi yake ya kusafiria na tiketi yake ya ndege.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post