MKANDARASI AFUNGWA JELA MIAKA 7 KWA UDANGANYIFU WA FEDHA


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu mkandarasi wa majengo, Alfred Ndeka (60) kifungo cha miaka saba jela baada ya kukutwa na hatia ya kujipatia Sh116 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Hukumu hiyo imetolewa jana Jumatano na Hakimu mwandamizi, Vicky Mwaikambo baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo 11 vilivyowasilishwa mahakamani hapo.

Mwaikambo amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo na anahukumiwa kifungo cha miaka saba jela ili iwe fundisho kwa wengine.

“Kutokana na ushahidi pamoja na vielelezo vilivyotolewa unadhibitisha ulipokea Sh116 milioni kwa njia ya udanganyifu huku ukijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria hivyo mahakama hii inakuhukumu kwenda miaka saba jela,” amesema Mwaikambo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527