MAREKANI NA TALIBAN WATIA SAINI MKATABA WA KUMALIZA VITA VYA AFGHAN VYA ZAIDI YA MIAKA 18 | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, February 29, 2020

MAREKANI NA TALIBAN WATIA SAINI MKATABA WA KUMALIZA VITA VYA AFGHAN VYA ZAIDI YA MIAKA 18

  Malunde       Saturday, February 29, 2020

Marekani na kundi la wanamgambo wa Taliban leo wametia saini makubaliano ya amani yanayolenga kumaliza vita vya miaka 18 nchini Afghansitan na kuwezesha Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini humo.Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Doha, Qatar.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo pamoja na msemaji wa kundi la Taliban mjini Doha, Suhail Shaheen walikuwepo wakati makubaliano hayo yaliposainiwa.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mike Pompeo ametoa wito kwa Taliban kuheshimu ahadi ilizotoa ikiwa ni pamoja na kukomesha mahusiano yake na makundi ya itikadi kali.

Chini ya mkataba huo Marekani itaanza kuondoa wanajeshi wake kwa makubaliano ya Taliban kuzuia mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Afghanistan.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post