JESHI LA POLISI NCHINI LATOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Jeshi la polisi  limewahakikishia wananchi kuwa hali ya ulinzi na usalama nchini ni shwari kwani uhalifu unaendelea kudhibitiwa.

Msemaji wa Jeshi la Polisi SACP- Davide A. Misime amesema kuwa licha ya hali ya usalama kuwa shwari yapo matukio ambayo yamesababisha vifo kwa watanzania wenzetu vilivyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali na tukio la waumini waliokuwa kwenye ibada ya maombi kule Mkoani Kilimanjaro kukanyagana na kusababisha vifo vya watu 20 na wengine takribani 16 kuumia sehemu mbalimbali na wanaendelea na matibabu.

“Tukio lilitokea Mkoani Kilimanjaro ni tukio baya kwani watanzania wenzetu walikwenda kwenye ibada lakini hawakutarajia wangepoteza maisha. Makongamano na ibada za maombi zimefanywa mara nyingi kupitia viongozi wa madhehebu mbalimbali na hakuna madhara yaliyotokea”. Amesema SACP- Misime.

Hata hivyo  SACP-Misime amesema kuwa Kutokana na hali hiyo ndiyo maana tukio hilo limechukuliwa hadi sasa kama taarifa ya vifo na siyo mauaji.

“Jeshi la Polisi kama ilivyoelezwa awali lilimkamata Boniface Mwamposa na wenzake walioandaa kongamano hilo la ibada na kuchukua maelezo yao. Pia uchunguzi wa kina unaendelea kufanywa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na pale ambapo itabainika kwamba kunakosa la jinai lilitendwa na kupelekea kutokea kwa vifo hivyo na majeruhi hao hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika kwa mujibu wa sheria”. Amesema SACP-Misime


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post