IGP SIRRO AZUNGUMZIA KUHUSU MAKAO MAKUU YA KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA (FFU) PAMOJA NA KUTENGWA ENEO KWA AJILI YA MAZOEZI


Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) nchini, Simon Sirro amemuagiza Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Kamishna Msaidizi wa Polisi, Paul Sanga ahakikishe anatenga eneo maalum jijini Dodoma litakalotumiwa na askari wa kikosi hicho kwa ajili ya mafunzo.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la polisi ambalo sasa linatumika kama Makao Makuu ya FFU.

Kwa upande wake Kamanda Sanga amemuhakikishia IGP Sirro kuwa watatekeleza maelekezo aliyowapatia.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527