IDADI YA WALIOKUFA KWA CORONA YAFIKIA 722 CHINA


Idadi ya vifo vinavyotokana na maambukizi ya mripuko wa virusi vya corona imeongezeka na kufikia watu 722, ikipindukia rekodi ya vifo vilivyotokana na mripuko mwingine wa virusi vinavyofanana na hivyo vya SARS ambavyo viliikumba China Bara na Hong Kong miongo miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa kamisheni ya afya ya taifa idadi nyingine ya watu 86 imepoteza maisha ambapo watano miongoni mwa hao wanatokea katika jimbo la Hubei, ambalo mripuko huko ulizuka Desemba. Kwa rekodi za kila siku kamisheni hiyo pia imesema visa 3,399 vimeripotiwa. 

Kwa hivi sasa zaidi ya watu 34,546 wameambukizwa virusi vyacoronakwa nchi nzima. Katika kipindi cha mwaka 2002 na 2003, ugonjwa wenye kufanana na huu unaosababaishwa na corona uliopewa jina la SARS ulisababisha vifo vya watu 650.

Meli ya starehe ya Japan Princess Diamond imekuwa ikiangaziwa zaidi katika kipindi hiki ambapo pia imeripotiwa visa vitatu vipya na kufanya jumla ya abiria wake 64 kuwekwa katika uangalizi maalumu kwa siku 14. Meli hiyo ilikuwa na jumla ya abiria 3,700. Ijumaa Rais Xi Jinping wa China alizungumza na Rais Donald Trump na kuitaka Marekani kushiriki haraka katika kukabiliana na mripuko wa virusi vya corona, na hasa kutokana na malalamiko ya baadhi ya nchi kuwazuia wasafiri kutoka China.

-DW


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post