HATIMA KESI YA HALIMA MDEE KUJULIKANA APRIL 1, 2020 | MALUNDE 1 BLOG

Friday, February 21, 2020

HATIMA KESI YA HALIMA MDEE KUJULIKANA APRIL 1, 2020

  Malunde       Friday, February 21, 2020

Hatima ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, anayekabiliwa na kesi ya uchochezi itajulikana Aprili Mosi kama ana kesi ya kujibu au la.

Hatua hiyo imefikiwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai kuwa kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kusikilizwa, lakini upande wa Jamhuri umefunga ushahidi wao na kwamba mashahidi watatu wanatosha kujenga kesi yao.

Hakimu Simba alisema upande wa utetezi uwasilishe hoja zao ndani ya siku 14 na upande wa Jamhuri uwasilishe majibu baada ya siku 14 nyingine.

Alisema mahakama yake itatoa uamuzi wa kama  Mdee ana kesi ya kujibu au la Aprili Mosi.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), iliyopo Mtaa wa Ufipa Wilaya ya Kinondoni, Mdee anadaiwa kutamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa “anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afungwe breki” kwamba kitendo ambacho kingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post