YANGA YATANGAZA KOCHA MPYA


Kocha Riedoh Berdien


Klabu ya Yanga imethibitisha kuingia mkataba na kocha Riedoh Berdien raia wa Afrika Kusini kuja kuongeza nguvu katika benchi la ufundi la klabu hiyo.

Berdien anakuja kuwa kocha wa viungo wa klabu hiyo huku pia akiwa ni kocha msaidizi wa pili wa klabu chini ya kocha mkuu aliyetangazwa mapema wiki hii, Luc Eymael.

Kocha huyo amewahi kufanya kazi na timu ya soka ya taifa ya Gambia, Botswana, Bangladesh, Trinidad na Tobago, timu ya wanawake ya taifa ya Afrika Kusini pamoja na klabu ya Chippa United ya nchini Afrika Kusini.

Pia Berdien ana uhusiano mzuri na kocha Luc Eymael kutokana na kuwahi kufanya kazi pamoja katika klabu ya Free State Stars ya nchini Afrika Kusini na inaaminika kuwa kocha Eymael ndiye aliyependekeza kusajiliwa kwa kocha huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post