ATUPWA JELA KWA KUMUINGIZIA UUME MDOMONI MTOTO ANYONYE DAR


Na Pamela Chilongola, Mwananchi 
 Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam imemuhukumu kifungo cha miaka 20 jela mkazi wa Kimara Stop Over, Liziki Kessy baada ya kukutwa na hatia ya kumwingiza uume wake kwenye haja kubwa na mdomoni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba ili aunyonye.

Hukumu hiyo imesomwa leo Jumatatu Januari 20, 2020 na Hakimu Mkazi, Hudi Hudi amesema mahakama hiyo imemtia hatiani mshtakiwa huyo baada ya kupitia mashahidi watano wa upande wa mashtaka huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi watatu akiwamo mshtakiwa mwenyewe.

Hudi amesema amezingatia shtaka hilo adhabu ya chini ni miaka 30 hivyo mahakama hiyo imemuhukumu mshtakiwa huyo kwenda jela miaka 20 .

Hudi amesema baada ya kupitia upande wa ushahidi wa mashtaka na ushahidi upande wa utetezi mahakama hiyo imebaini mshtakiwa huyo alimfanyia tendo la aibu kwa mtoto huyo.

Amesema kutokana na mtoto (muathirika) huyo kuieleza mahakama jinsi mshtakiwa alivyomwita na kumpeleka kwenye jumba bovu huku akimvua kaptura na kuanza kumuingizia uume wake kwenye haja kubwa na alipopiga kelele ndipo mshtakiwa huyo aliuingiza uume kwenye mdomo wa mtoto huyo.

"Ushahidi wa muathirika umeungana na ushahidi aliyoutoa mama yake mzazi pamoja na daktari wa hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala ambaye alibaini mtoto huyo alikuwa na michubuko kwa jinsi ilivyo kama kuna kitu kisicho na ncha kimeingizwa sehemu ya haja kubwa," amesema Hudi.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527