UTURUKI YAMUONYA JENERALI HAFTAR DHIDI YA MASHAMBULIZI ZAIDI


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan amesema nchi hiyo haitasita kumpa fundisho Kamanda wa Wapiganaji wa Mashariki mwa Libya, Jenerali Khalifa Haftar iwapo vikosi vyake vitaendelea kuishambulia serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa mjini Tripoli. 


Urusi na Uturuki zilikuwa zinajaribu kupata mkataba wa kudumu wa kusitisha mapigano ambapo mbabe huyo wa kivita wa Libya alitakiwa kutia saini ambapo aliomba muda hadi leo Jumanne kufikiria suala hilo lakini baadaye imefahamika kuwa ameondoka mjini Moscow bila kutia saini makubaliano hayo.


Mazungumzo ya jana Jumatatu yalitarajiwa kuweka rasmi mkataba wa muda wa kusitisha mashambulizi ulioafikiwa siku ya Jumapili lakini mkataba huo haukutekelezwa kikamilifu na kuna ripoti ya mapigano kuendelea nchini Libya.

Taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta lina serikali mbili pinzani. Serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inayoongozwa na al-Serraj mjini Tripoli na nyingine yenye makao yake katika mji wa Tobruk, Mashariki mwa Libya inayoongozwa na Haftar.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post