VIGOGO WA CHAMA CHA USHIRIKA NGARA FARMERS WAKIFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI


Na Ashura Jumapili- Malunde 1 blog Bukoba
Jeshi la polisi mkoani Kagera limewafikisha katika mahakama ya hakimu mkazi ya Wilaya ya Bukoba vigogo wanne wa Chama Cha Ushirika cha Ngara Farmers mkoani Kagera kwa tuhuma mbalimbali makosa ya ubadhilifu wa fedha za wakulima,kula njama za kutenda kosa,matumizi mabaya ya ofisi na uhujumu uchumi na kusomewa mashtaka tisa.

Akizungumza mahakamani hapo leo,Wakili wa Serikali Haruna Shomali amewataja watuhumiwa hao mbele ya Mahakama kuwa ni Thomson Soyongwe aliyekuwa Mwenyekiti, Paschal Minani aliyekuwa Meneja,Paschal Kangeze aliyekuwa Mhasibu na Bazilius Thomasi ni aliyekuwa Mtunza Stoo ambapo walisomewa mashtaka yanayowakabili mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi wa Bukoba John Kapokolo.

Watuhumiwa hao wanadaiwa kukisababishia chama hicho hasara ya zaidi ya shilingi milioni 14 ambapo makosa hayo yalitendeka kwa nyakati tofauti kwa kipindi cha kati ya mwaka 2012 na 2014 wakati wakiwa viongozi wa chama hicho.

Baada ya hakimu Kapolo kusikiliza hoja za Jamhuri alisema kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo mpaka mahakama ya juu kutokana na mashtaka yanayowakabili likwemo la uhujumu uchumi ambalo mashitaka yake yanazidi kiasi cha milioni kumi na haina mamlaka ya kutoa dhamana.

Washtakiwa wamerudishwa rumande ambapo kesi hiyo itatasikilizwa Februari 11 mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527