BOB WINE AKAMATWA TENA UGANDA


Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda, Robert Kyagulani, maarufu Bobi Wine, leo Januari 6, 2020, Jeshi la Polisi nchini humo limemkamata na kisha kurusha mabomu ya machozi kwa lengo la kuzuia mkutano wake, uliokuwa umepangwa kufanyika eneo la Gayaza, Kyadondo Mashariki.


Bobi Wine alikamatwa pamoja na wabunge wengine Asuman Basalirwa, Latif Ssebagala,Waiswa Mufumbira na mwenyekiti wa baraza la Kasangati na kwa sasa wanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kasangati.

Gazeti la The Observer limemnukuu Basalirwa akisema walikuwa wakiendesha gari la Kyagulanyi kabla ya polisi kuwazuia katika eneo la Kasangati na kuwapeleka katika kituo cha polisi. Kyagulanyi alikuwa akitarajiwa kuzindua mikutano ya mashauriano kuhusu malengo ya urais kwa uchaguzi mkuu ujao.

Polisi wamedai kuwa ilibidi kuuzuia mkutano huo kwa sababu ulipangwa kufanyika kwenye eneo la wazi, wakati mikutano ya namna hiyo hufanyika ndani ili kutoingilia shughuli za watu wengine.

Pia polisi wamedai kuwa hakukuwa na vyoo vya kutosha kwa ajili ya wageni waliokuwa wakitarajiwa.

Mbunge huyo aliiandikia tume ya uchaguzi kabla ya krisimasi akieleza nia yake ya kufanya mkutano kitaifa kuhusu nia ya kuwania urais. Ingawa alitoa taarifa kwa tume hiyo, ambayo ilimruhusu, imesema hakutimiza vigezo vingine kama vinavyoelezwa kwenye sheria.

Bobi Wine ameeleza nia yake ya kuwanida urais dhidi ya rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post