SIMBA KUTOA TAMKO LEO KUHUSU TUHUMA ZA MCHEZAJI WA YANGA, RAMADHAN KABWILI


Uongozi wa Simba umesema kuwa leo utalitolea ufafanuzi suala la madai ya mlinda mlango wa Yanga, Ramadhan Kabwili kudai kuwa aliahidiwa gari aina ya Toyota IST endapo angefanya makusudi ya kutocheza mchezo wao wa msimu uliopita 2018/19.

Kabwili alidai kuwa, kuna watu ambao anadai walikuwa ni viongozi wa Simba walimfuata na kumtaka afanye makusudi kwenye mechi zake apate kadi ya njano ili asipangwe kwenye kikosi kwa kuwa alikuwa na kadi mbili za njano.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa watajibu tuhuma alizotoa mchezaji huyo ila cha msingi awe na ushahidi.

" Tutajibu tuhuma za jumla jumla alizotoa huyu mchezaji kwa klabu yetu. Muhimu wakati huu akijiandaa kikamilifu na ushahidi wa hizo tuhuma," .


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527