HALI YA JANGWANI DAR SI SHWARI,BARABARA YAFUNGWA MAJI BALAA

Na Andrew Chale - Dar es salaam

Hali halisi eneo la jangwani jijini Dar es salaam, mamlaka zimefunga rasmi matumizi ya barabara ya Morogoro eneo la magomeni kuelekea katikati ya jiji kufuatia kujaa kwa maji eneo la jangwani.


Kwa hali hiyo imesababisha msongamano mkubwa wa watu karibu maeneo yote ya jiji ambapo njia ya kuelekea Kinondoni Mkwajuni eneo la Magomeni Morocco  pia maji yamejaa na msongamano wa magari na watu ni mkubwa pia.

Katika hali nyingine Basi la kampuni ya Tahmeed limekwama  katika eneo la Jangwani baada ya kujaribu kukatisha wakati wa maji hayo yakiwa tayari yamejaa.

Baadhi ya wananchi wameiomba Serikali kuhakikisha wanaleta mpango maalum wa  daraja utakaosaidia kuondoa usumbufu wanaopata kila wakati wa eneo hilo linapojaa maji.

Barabara hiyO imefungwa kuanzia majira ya saa 12 asubuhi ambapo jeshi la Polisi limeweka ulinzi mkali kwa raia kutokatisha eneo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post