MTU MFUPI ZAIDI DUNIANI AFARIKI DUNIA

Khagendra Thapa Magar enzi za uhai wake
Mtu mfupi zaidi duniani ambaye anaweza kutembea kama ilivyothibitishwa na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness amefariki hospitalini Nepal akiwa na umri wa miaka 27.

Khagendra Thapa Magar, kutoka wilaya ya Baglung alikuwa na urefu wa sentimita 67.08cm sawa na futi mbili na nchi 4..

Nduguye aliambia chombo cha habari cha AFP kwamba alifariki siku ya Ijumaa baada ya kuugua homa ya mapafu.

Kitabu cha rekodi za Guiness kilituma risala za rambi rambi kwa bawana Magar kikisema kwamba hakuwacha udogo wake kumzuia kupata maisha bora duniani.

Bwana Magar alitambulika kuwa mtu mfupi zaidi duniani wakati wa sherehe za kuadhimisha mwaka wake wa 18 wa kuzaliwa mwaka 2010.

Katika sherehe iliowaleta pamoja maafisa wakuu kutoka maeneo tofauti alisema:. Sijichukulii kuwa mtu mdogo.

''Mimi ni mtu mkubwa , natumai kwamba taji hili litanifanya kuthibitisha hilo ili niweze kupata nyumba nzuri na familia yangu'' , alisema wakati huo.

Kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness kina orodha mbili za watu wafupi - wanaotembea na wasio tembea.

Raia wa Ufilipino Junrey Balawing ambaye hawezi kutembea ama hata kusimama bila usaidizi ndio mtu mfupi zaidi duniani asiyeweza kutembea. Akiwa na urefu wa sentimita 59.93.

Bwana Magar alipoteza taji lake akiwa mtu mfupi zaidi duniani kwa raia wa Nepal Chandra Bahadur Dangi ambaye alikuwa na urefu wa sentimita 54.6.

Hatahivyo, alihifadhi taji lake kufuatia kifo cha bwana Dangi 2015.

Bwana Magara kwa mara ya kwanza alionekana na muuzaji mmoja wakati alipokuwa na umri wa miaka 14 na kuchukuliwa katika maonyesho ya eneo hilo ambapo watoto walilazimika kulipa fedha ili kupigwa picha naye.

Baada ya kutambulika na kitabu cha rekodi za dunia cha Guiness 2010, alisafiri maeneo mbalimbali duniani na kuonyeshwa katika vipindi vya runinga Ulaya na Marekani . Pia ndiye aliyekuwa sura rasmi ya kampeni za italii huko Nepal .

Craig Glenday, Muhariri wa kitabu cha rekodi za Guiness alisema kwamba alijawa na majonzi aliposikia habari za kifo cha bwana Magar.

''Alikuwa na tabasamu nzuri ambayo ilimvutia kila mtu aliyekutana naye'', alisema.

Rekodi ya mtu mfupi zaidi duniani anayetembea hivi sasa inashikiliwa na Edward Hernandez wa Colombia ambaye ana urefu wa sentimita 70.21.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527