MMILIKI MABASI YA SAHARA AKUTWA AMEKUFA GESTI

Mfanyabiashara na mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) mkazi wa Usangi Mkoani Kilimanjaro, leo Jumapili Januari 5, 2020 amekutwa amekufa kwenye moja ya nyumba ya wageni iliyopo Mtaa Dar es Salaam Mjini Moshi.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Tanzania, James Manyama amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Amesema mfanyabiashara huyo alikuwa na rafiki yake wa kike chumbani, lakini baada ya kuona mwenzake anaishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu puani na mdomoni akakimbia.

“Huyu Mfanyabiashara alikuwa na rafiki yake wa kike kwenye chumba cha wageni huko Dar es Salaam street, baada ya kuona ameishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu mdomoni alitoroka, amedai Kamanda Manyama.

Aidha, amesema baada ya kupata taarifa na kufika eneo la tukio na kulipekua gari la Msangi kulikutwa dawa ya kienyeji ambayo imechukuliwa kwa uchunguzi.

Amesema Mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Mkoa Mawenzi kwa uchunguzi zaidi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post