Picha : DC MBONEKO AFANYA ZIARA KUKAGUA MAENDELEO YA SHULE, TINDE NA NSALALA, ASHANGAZWA NA UTORO WA WANAFUNZI




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya wanafunzi katika shule za msingi Kata ya Tinde na Nsalala, pamoja na shule ya Sekondari ya Tinde, huku akikagua miundombinu ya shule hizo, ikiwamo na ujenzi wa Bwalo katika shule ya Sekondari ya wasichana Tinde Girls zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mboneko amefanya ziara hiyo leo Januari 30, 2019, akiwa ameambatana na maofisa elimu Kata na wilaya wa shule za msingi na Sekondari kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Akiwa katika shule hizo za msingi na Sekondari ya Tinde, alikumbana na changamoto ya utoro kwa wanafunzi, ambapo alipoaliwauliza wenzao wako wapi wakabainisha wamekwenda mashambani kulima.

Kutokana na hali hiyo mkuu huyo wa wilaya, amewaagiza watendaji wa Kata na waratibu elimu, kufuatilia wanafunzi wote ambao ni watoro wahudhuRie shule, na wale ambao wazazi wao wataonekana kukaidi kuendelea kuzuia watoto wao kwenda shule na kuwapeleka kwenye mashamba wachukuliwe hatua.

“Haiwezekani wanafunzi katika kipindi hiki cha masomo wapo mashambani kwenye majaruba wanalima mpunga, huku wenzao wakiendelea na masomo tena wengine ni darasa la saba ambao mwaka huu wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, naagiza wafuatiliwe wote warejee shule,” amesema Mboneko.

“Natoa wito pia kwa wazazi wawekeze watoto wao kwenye elimu, Serikali inatoa elimu bure na kulipia gharama zote, lakini baadhi yao hawapendi kusomesha watoto shule na hatimaye kuwapeleka mashambani kulima majaruba, huku wenzao wakiendelea na masomo mwisho wa siku wanakuja kufeli mtihani na kupoteza dira ya maisha,”ameongeza.

Katika hatua nyingine amewataka wanafunzi kuongeza bidii kwenye masomo yao ili wapate kufaulu na kutimiza ndoto zao, pamoja na wasichana kuacha tabia ya kupenda vitu vidogo na hatimaye kuingia kwenye mahusiano na kuambulia ujauzito, huku akiwasihi pale wanapotaka kuozeshwa ndoa za utotoni watoe taarifa ili ndoto zao zipate kuokolewa.

Naye Ofisa elimu Kata kutoka Kata ya Tinde, Vumilia Mauna, amesema tatizo hilo la wanafunzi kuwa watoro na kwenda kulima mashambani, tayari walishakaa kwenye kikao cha Kata, kuwa mwanafunzi akifikisha siku tatu hayupo shule wanamfuata nyumbani kwao na kumrejesha shule, huku wakimuonya mzazi wake.



TAZAMA PICHA HAPA CHINI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wanafunzi katika shule ya Msingi Tinde 'A' na kuwataka wasome kwa bidii na kuacha utoro kwa kwenda kulima majaruba. Picha na Marco Maduhu - Malunde 1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wanafunzi katika shule ya Msingi Tinde 'B' na kuwataka wasome kwa bidii na kuacha utoro kwa kwenda kulima majaruba.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wanafunzi wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Ng'wankanga na kuwataka wasome kwa bidii na kuacha utoro kwa kwenda kulima majaruba.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na wanafunzi wa Darasa la Saba katika shule ya Msingi Nshishinulu na kuwataka wasome kwa bidii na kuacha utoro kwa kwenda kulima majaruba ili watimize ndoto zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya Tinde na kuwataka wasome kwa bidii na kuacha utoro ili watimize ndoto zao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Sekondari ya wasichanaTinde Girls na kuwataka wasome kwa bidii na ili watimize ndoto zao.

Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akitoa maelekezo kwa walimu, watendaji wa Kata na Maofisa elimu, kudhibiti utoro kwa wanafunzi mashuleni.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza na kamati ya shule pamoja na uongozi wa shule ya msingi Nshishinulu na kuwataka wadhibiti utoro kwa wanafunzi.

Kamati ya shule pamoja na uongozi wa shule ya msingi Nshishinulu wakiwa kwenye kikao na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa ofisi ya walimu katika shule ya Msingi Nsalala.


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa Bwalo katika Shule ya Sekondari ya wasichana Tinde (Tinde Girls).

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa Bwalo katika Shule ya Sekondari ya wasichana Tinde (Tinde Girls).

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na wanafunzi katika shule ya Sekondari ya wasichana Tinde (Tinde Girls) na kuwataka wasome kwa bidii ili watimize malengo yao.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipiga picha ya pamoja na wanafunzi katika shule ya Sekondari ya wasichana Tinde (Tinde Girls).

Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527