KOCHA WA YANGA ACHUKIZWA NA MBWEMBWE ZA MORRISON..... ''KITENDO ALICHOFANYA NI KUWAKOSEA HESHIMA WAPINZANI'' | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, January 28, 2020

KOCHA WA YANGA ACHUKIZWA NA MBWEMBWE ZA MORRISON..... ''KITENDO ALICHOFANYA NI KUWAKOSEA HESHIMA WAPINZANI''

  Malunde       Tuesday, January 28, 2020
Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael amesema hapendi kuona mchezaji wake, kiungo Bernard Morrison akiwadhalilisha wapinzani wake kwa staili yake ya uchezaji.


Kauli hiyo ameitoa  Januari 26, 2020 baada ya kumalizika kwa mchezo wake na Timu ya Tanzania Prisons katika  Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation Cup (ASFC)' ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 2-0,

Kocha Eymael amesema kuwa ameshaoongea na mchezaji huyo juu ya aina yake ya mchezo ambao unawadhalilisha wapinzani.

"Mimi sipendezwi kuona mtu anawadhalilisha wengine, ukifanya vile Ulaya utafanyiwa 'tackle' ya hatari sana. Ukiangalia Liverpool, Mo Salah anaweza kufanya hivi?, Sadio Mane anafanya hivi? hapana na mimi nimeshaongea na Morrison nimemwambia sipendi staili hii", amesema Eymael na kuongeza kuwa;

"Mashabiki wanapenda kuona mchezaji akifanya hivyo lakini kwangu mimi ni kutowaheshimu wapinzani na nimeshamwambia Bernard Morrison",

Katika michezo miwili ya Yanga, Morrison ametokea kupendwa na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na aina ya uchezaji wake uliojaa mbwembwe za kupanda juu ya mpira huku mashabiki wa timu hiyo wakimpa sifa lukuki na kudai Morrison ni wakina Chama 500 (Chama ni mchezaji wa Simba).


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post