Tanzia : MWANDISHI WA HABARI AKUTWA AMEFARIKI DUNIA DAR


Mwandishi wa habari Deouglas David (pichani) amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake eneo la Buguruni jijini Dar es salaam.

Inaelezwa kuwa Deouglas amekutwa amefariki dunia leo Jumatatu Januari 27,2020 chumbani kwake eneo la Buguruni baada ya majirani zake kuanza kuhisi harufu kutoka chumbani kwake ndiyo wakafanya utaratibu wa kufungua mlango kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ya mtaa chini ya usimamizi wa jeshi la polisi kituo Polisi Buguruni.



Mashuhuda wanasema walipofungua mlango waliona mwili wa Deouglas David ukiwa umelala kitandani kwa takribani siku tano.

Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Ilala, Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

“Taarifa walizipata kutoka kwa majirani, baada ya kupita siku tatu bila kumuona na kusikia harufu kali ikitoka chumbani mwake na ndipo walipoamua kuvunja mlango.

“Mwili wake ulikutwa umelala kifudifudi kitandani kwake ukiwa umeharibika tayari, majirani wanasema waliamua kuuvunja mlango baada ya kutomuona kwa siku tatu, lakini pia kusikia harufu iliyokuwa ikitokea chumbani mwake na wanasema marehemu alikuwa na ugonjwa wa kifafa,” amesema ACP Magomi.

Mwili wa marehemu  utasafirishwa kesho tarehe 28/1/2020 kuelekea Sumbawanga mkoani Rukwa kwa ajili ya mazishi.

Enzi za uhai wake Deouglas David aliwahi kufanya kazi katika vyombo vya habari vya DARMPYA BLOG&TV ONLINE, LEMUTUZ BLOG &TV ONLINE na mpaka kifo kinamkuta alikuwa anafanya kazi kwa kujitolea katika kituo cha TBCONLINE


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post