KESI YA KUMUONDOA TRUMP MADARAKANI: MASENETA 100 WAAPISHWA

Maseneta 100 wa Marekani wameapishwa Alhamisi kama baraza la mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump.


Hakimu mkuu wa mahakama ya juu zaidi John Roberts aliapisha maseneta kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo.

Wiki zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi. Kesi hiyo imepangiwa kuanza kusikilizwa Januari 21.

Hakimu Roberts aliwauliza maseneta, " Je mnaapa ya kwamba katika kesi inayomkabili Donald Trump, Rais wa Marekani, ambayo inayongoja kusikilizwa, mutatenda haki bila upendeleo kulingana na katiba, Mungu awasaidie?"

Wabunge wakajibu "Ndio" kabla ya kila mmoja wao kusaini kitabu walichochukulia kiapo. Kiongozi wa waliowengi wa Republican Mitch McConnell, kisha akaahirisha kikao cha kutathmini iwapo Donald Trump ana kesi ya kujibu na kutangaza kwanza kesi hiyo itaanza kusikilizwa Jumanne, 13:00 EST (18:00 GMT).

Bwana Trump anashtumiwa kwa kutumia vibaya madaraka na kuingilia bunge. Hata hivyo amekanusha kutekeleza makosa hayo na kusema kwamba kesi dhidi yake ni madai dhidi yake ni ya uongo

BBCDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post