JENERALI QASSEM SOLEIMANI WA JESHI LA MAPINDUZI LA IRANI ALIYEUAWA NA MAREKANI LEO NI NANI HASA?


Tangu miaka ya 80, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya kikurdi nchini Iran- kitengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.


Kwa sehemu kubwa aliwakilisha taswira ya ustahamilivu wa kitaifa katikati ya miongo minne ya mbinyo wa Marekani.

Jenerali Soleimani amekuwa shujaa nchini Iran kutokana na juhudi zake za kuipinga Marekani.

Kwa Marekani na Israel  Soleimani alikuwa kiongozi hatari, aliye nyuma ya vikosi vinavyoungwa mkono na Iran na anayehusika na wapiganaji wanaoitetea serikali ya rais Bashar Al Assad nchini Syria.

Kadhalika alibebeshwa wajibu wa vifo vya wanajeshi wengi wa Marekani nchini Iraq.

Soleimani alivishinda vishindo vya vita ya muda mrefu ya Iran dhidi Iraq miaka ya 1980 ili kuchukua nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds kilicho sehemu ya kikosi kipana cha walinzi wa mapinduzi ya Iran.

Kikosi cha Quds ndiyo kinahusika na kampeni zote za kijeshi za Iran kwenye mataifa ya kigeni.

Jenerali huyo hakuwa akifahamika na wengi nchini Iran hadi mwaka 2003 wakati Marekani ilipoivamia kijeshi Iraq.

Wasifu na umashuhuri wake uliimarika hatua iliopelekea maafisa kadhaa wa Marekani kutoa wito wa kuuliwa kwake.

Muongo mmoja na nusu baadae Soleimani alifikia kuwa kamanda maarufu wa vita nchini Iran kiasi akipuuza miito ya umma kumtaka aingie kwenye siasa.

Kwa jenerali Soleimani nafasi ya kisiasa haikuwa na umuhimu mkubwa kwa sababu kutokana na ushawishi wake jeshini alifikia nafasi ya kuwa mtu mwenye nguvu nchini Iran pengine kuliko utawala wa kiraia.

Kifo chake kimekuja baada ya kuzushiwa mara kadhaa kufikwa na umauti. Soleimani alizaliwa mwezi Machi mwaka 1957 na kukulia kwenye mji wa kihistoria wa Rabor nchini Iran.

Jina lake liianza kuzingatiwa alipopewa nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds na kujenga ukaribu  na kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei kiasi wakati mmoja Kiongozi  huyo alishiriki na kufungua dhifa ya harusi ya binti ya Jenerali Soleimani.

Akiwa mkuu wa kikosi cha Quds Soleimani alisimamia operesheni za kijeshi nje ya Iran na kuingia kwenye uhasama na Marekani wakati wa vita vya Iraq akionekana kuwa mfadhili wa makundi ya wanamgambo wa kishia.

Mwaka 2007 Marekani na Umoja wa Mataifa walimjumisha Soleimani katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo lakini aliendelea kusafiri maeneo mbali mbali duniani.

Umashuhuri uliimarika zaidi wakati wa vita vya Syria na kutanuka kwa kundi linalojiita dola la kiislam. Iran ilimtuma Soleimani mara kadhaa nchini Syria kuongoza mashambulzii dhidi ya kundi la IS na makundi yanayopinga utawala wa Bashr Al Assad.

Jenerali huyo alipata mafanikio makubwa kwenye mapambano ya ardhini na alikuwa alama ya ushindi katika vita dhidi ya IS na kuendelea kulipa nuru jina lake, zaidi katika viwambaza vya dola na mioyoni mwa raia wengi wa Iran.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527