AFISA MTENDAJI MKUU BRELA AANZA KAZI RASMI


Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana wadau wa BRELA alipokua akitembelea Ofisi za Idara na Vitengo mbalimbali baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (Mwenye tai nyekundu) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Leseni BRELA Bw. Andrew Mkapa mara baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Uwezeshaji Bw. Bakari Mketo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa akifafanua jambo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (Mbele) Akizungumza na Wakurugenzi wa Idara na Vitengo Mbalimbali BRELA mara baada ya kuwasili leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.

Na Robertha Makinda - BRELA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Godfrey Nyaisa amewasili rasmi katika kituo chake kipya cha kazi leo Januari 23, 2020 BRELA Ofisi Kuu Mnazi mmoja, Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili katika BRELA Ofisi Kuu Bw. Nyaisa amepata wasaa kukaa kikao kifupi na Menejimenti, kutambulishwa kwa wafanyakazi pia kukutana na baadhi ya wadau wa BRELA waliokua wakipata huduma kwa siku ya leo.

Katika maneno yake ya utambulisho kwa wafanyakazi wa BRELA amewataka wampe ushirikiano na kufanya kazi kwa bidii.

“Wafanyakazi wanzangu naomba kwa kipindi hiki tushirikiane ili tuweze kufanya kazi za serikali ni matumaini yangu kila mmoja atasimama katika nafasi yake na kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha azma ya Tanzania ya Viwanda na kuwa nchi ya uchumi wa kati”, alisema Bw. Nyaisa.

Aidha alipokua akizungumza na wadau wa BRELA waliokuwa wakipata huduma siku ya leo, amewaomba waweze kuwa wavumilivu kwa kwa kipindi hiki wakati BRELA inajipanga kutoa huduma bora na kuondoa malalamiko yaliyopo, alibainisha Bw. Nyaisa.

Bw. Nyaisa aliteuliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA tarehe 19 Januari, 2020 akichukua nafasi ya Bi. Loy Muhando aliekuwa akikaimu nafasi hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527