BASI LAPINDUKA MOROGORO....9 WAJERUHIWA


Watu 9 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni Kidinilo kuacha njia jana  Alhamisi Januari 9, 2020 na kupinduka eneo la Mangae barabara ya Morogoro Iringa huku chanzo kikitajwa ni uzembe na mwendokasi.

Basi lililokuwa kilitokea Ifakara kwenda Dar es Salaam lilikuwa na abiria 68  kwamba majeruhi watatu hali zao sio nzuri kutokana na majeraha makubwa waliyoyapata na wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, ameeleza chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Basi la Kidinilo kutaka kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari, Dereva huyo anaitwa Shabani Sultan (54) amekamatwa wakati akijaribu kutoroka kwa kutumia Bodaboda. 


“Kati ya majeruhi tisa walionusurika kwenye ajali ya basi la Kidinilo, wawili wamevunjika miguu, mmoja hali yake si nzuri, wengine wamepata majeraha ya kawaida wanapatiwa matibabu" - RPC, Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527