BABU AVAMIA BENKI, AIBA PESA NA KUZIGAWA KAMA ZAWADI AKISEMA 'MERRY CHRISTMAS'


Bwana mmoja mwenye ndevu nyeupe amefanya uvamizi wa benki siku mbili kabla ya Krismasi na kuzirusha juu kwa furaha na kuwatakia kheri ya sikukuu wapita njia, mashuhuda wameeleza.

Polisi wamethibitisha "mwanaume mzee wa kizungu" alivamia benki ya Academy mjini Colorado Springs, Marekani siku ya Jumatatu.

"Aliiba pesa benki, akatoka nje na kuzitawanya kwa watu," shuhuda Dion Pascale alikiambia kituo cha Colorado's 11 News.

"Alianza kurusha fedha kutoka kwenye begi na kisha akaanza kusema, 'Merry Christmas!'"

Kwa mujibu wa mashuhuda, mtuhumiwa huyo akapiga hatua chache kutoka benki na kuketi mbele ya mkahawa wa Starbucks akisubiri kukamatwa.

Katika hali ambayo inaweza kuwa ya kustaajabisha kwa wakazi wa Afrika Mashariki, wapita njia wanaripotiwa kuwa walichota fedha zote zilizozagaa na kuzirudisha benki.


Polisi hawadhani kuwa alikuwa na usaidizi wowote.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post