WAFUNGWA 293 KUTOKA MAGEREZA YA MKOA WA DAR ES SALAAM WAACHIWA HURU KWA MSAMAHA WA RAIS MAGUFULI

Jumla ya Wafungwa 293 kutoka magereza Ya Ukonga, Keko,Segerea na Wazo Hill  jijini Dar es salaam leo wameachiwa huru kwa Msamaha wa Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli alietoa Msamaha kwa Wafungwa 5,533 waliokuwa wakitumikia kifungo kwenye magereza mbalimbali Nchi nzima.


Wafungwa hao wameachiliwa huru leo Mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Abubakar Kunenge, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam ambapo kwa pamoja wamewataka walioachiliwa huru kwa msamaha wa Rais kuhakikisha hawarudii kufanya makosa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es salaam Kamishina Msaidizi wa Magereza Julius Mtambala amesema kati ya Wafungwa hao 293 walioachiliwa huru 130 wanatoka Gereza la Ukonga,54 Gereza la Keko, 74 Gereza la Segerea na 35 wanatoka Gereza la Wazo hill.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post