WAASI WA ADF WAUA WATU 22 NCHINI CONGO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, December 16, 2019

WAASI WA ADF WAUA WATU 22 NCHINI CONGO

  Malunde       Monday, December 16, 2019

Waasi wa kundi la ADF wameishambulia tena wilaya ya Beni Kaskazini mwashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kuuwa watu 22 katika tarafa za Ndombi na Kamango.

Wakaazi wa wilaya ya Beni kwa mara nyingine wanahesabu maiti za wapendwa wao waliouawa kinyama na waasi wa ADF. 

Mauwaji haya yanaendelea wakati jeshi la serikali linaendesha operesheni  dhidi ya ADF, lakini wadadisi wa masuala ya usalama wanasema kuna uzembe katika uongozi wa jeshi hasa katika operesheni zinazotajwa na jeshi la Serikali kuwa ndio za mwisho kufanyika katika eneo hili, ili kuwatokomeza waasi wa ADF wanaowauwa watu kila uchao.

Ikumbukwe kuwa, katika ziara yake mjini Beni, na alipotangaza kwamba operesheni kabambe zitaanzishwa katika eneo hilo dhidi ya waasi wa ADF, rais FĂ©lix Tshisekedi aliwahi kuwaahidi wakaazi, kwamba waasi hao watatokomezwa kabla ya sherehe za Krismasi pamoja na mwaka mpya. Lakini ahadi hiyo inaonekana kubakia kuwa ndoto tu.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post