TANGA UWASA : MITA ZA LUKU ZITAPUNGUZA MADENI SUGU

 Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanga Uwasa Devota Mayala akizungumza wakati wa mkutano huo
 AFISA Uhusiano Msaidizi wa  Tanga Uwasa Anna Makange akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo


 Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanga Uwasa Devota Mayala akigawa vipeperushi wakati wa mkutano huo
Msimamizi wa Mtandao wa Maji Tanga Uwasa George Mbalai akigawa vipeperushi kwa wananchi wakati wa mkutano huo
 Mkazi wa Kata ya Mwanzange Mashaka Shabani akichangia kwenye mkutano huo
 Sehemu ya wananchi wa Kata ya Mwanzange Jijini Tanga wakifuatilia mkutano huo
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeeleza kwamba ufungaji wa mita za luku kwa wananchi na kwenye baadhi ya Taasisi za Serikali utasaidia kupunguza madeni na kuondoa kero.


Hayo yalisemwa  na Afisa Huduma kwa Wateja wa Tanga Uwasa Devota Mayala wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwanzange Jijini Tanga kwenye zoezi la uelimishaji kuhusu huduma zao.


Elimu hiyo pia ilitolewa kuhusiana na bili namna ya kutasfiri bili ambazo na namna zinavyopatikana ikiwemo matumizi sahihi ya maji ili waweze kuondokana na malalamiko ya kuletewa bili kubwa.


“Lakini niwaambieni wananchi suala mita za luku au limaku kwa upande wao Tanga Uwasa hivi sasa tupo kwenye majaribio tunafunga kwa baadhi ya Taasisi na wale wenye madeni sugu nia ni kutumia mita kupunguza madeni”Alisema


Alisema kwa sababu pia kwa mtu wa kawaida lengo la kupunguza madeni na kuondoa kero kwa wananchi ambao wanaona hawatumii bili ambazo ni sahihi na hivyo uwepo wa mfumo huo utawezesha kulipia huduma hiyo kabla ya kulipia.


Hata hiyo alisema kwamba kwa sasa tumezifunga kwa Tassisi kubwa na wateja wadaiwa sugu na bado wapo kwenye majaribio na wataangalia jinsi zinazofanya kazi lakini changamoto zake ni ikitokea itilafu ya aina yoyote kwenye mita mteja anakosa huduma hiyo.


“Kwani baadhiya mita hizo zinajifunga zenyewe kama ukikosea kufanya malipo mara ya pili zinaweza kujifunga zenyewe hivyo wanahitaji wataalamu ambao ikitokea itilafu wanaweza kuwasaidia kutatua hili kwa wakati “Alisema


Awali akizungumza wakati wa zoezi hilo la uelimishaji Afisa Ankra Msaidizi wa Tanga Uwasa Ausi Anthony alisema mita hizo zimeanza kufungwa kwa taasisi kubwa na mita zina gharama kidogo hivyo wakiwafungia wateja wa kawaida hakuna kiasi chochte wanachoweza kutoa.


Naye kwa upande wake mkazi wa Mwanzange Jijini Tangaa Mashaka Shabani alisema kwamba ufungaji wa mita hizo utakuwa mkombozi kwao kwani utawasaidia kuweza kutumia maji kwa uangalifu mkubwa ambao utakuwa chachu.


Alisema kwani mfumo huo utakuwa kama wanavyofanya kwenye suala la umeme kwa kulipia kabla ya kuanza kutumia na hivyo mtumiaji kuwa mamini na matumizi yake ya kila siku.


Naye kwa upande wake Beatrice Benjamini ambaye ni mkazi wa Mwanzange Jijini Tanga alisema bili inaweza kuja kubwa ukashindwa kulipia kutokana na kukosa fedha lakini uwepo wa mfumo wa mita za luku utawawezesha kuwa makini na kujiandaa na malipo muda wowote malipo yanapokwisha.


“Hivyo naomba kama inawezekana kwenye suala la maji kulipia tulipe kama luku tunavyolipia kwa Tanesco hivyo watuharakishie kwa sasa tuletewe mfumo huo kuweza kuwarahisishia “Alisema.


Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post