RAIS WA TFF WALLACE KARIA AMECHAGULIWA KUWA RAIS MPYA WA CECAFA

Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia amechaguliwa kuwa Rais mpya wa baraza la vyama vya soka na vilabu vya Afrika Mashariki maarufu kwa jina la CECAFA.


Karia amechaguliwa kuwa Rais wa CECAFA katika mkutano mkuu wa CECAFA uliyofanyika leo Lugogo jijini Kampala nchini Uganda.

Karia atadumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne akichukua nafasi ya Mutasim Gafaar kutokea Sudan aliyetawala kwa kipindi cha miaka minne katika nafasi ya Urais wa CECAFA.

Pia katika mkutano huo imeshuhudiwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka na Vilabu Afrika Mashariki na Kati CECAFA, Nicholas Musonye akiachia ngazi katika nafasi yake hiyo baada ya kuhudumu kwa miaka 20.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post