RAIS MSTAAFU KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA MAMA WA MWENYEKITI WA CCM MKOA MOROGORO


Mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro na Wilaya zake, wanachama na wakereketwa wa CCM, wanachama wa vyama mbali vya siasa, viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wakiongozwa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete   24 Disemba 2019 wamehudhuria na kushiriki mazishi ya *Mama mzazi wa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogeris

Mama Theodora Vasos Kalogeris amefariki dunia Jumapili 22 Disemba 2019 Hospital ya Chuo cha Kilimo (SUA) Morogoro na kuzikwa leo alasiri makaburi ya Kola Hill Morogoro Mjini.

Mapema viongozi na wanachama walipata kuaga mwili kisha kufanyiwa ibada fupi nyumbani kwake Mji mpya na baadae kufuatiwa na Ibada ya mazishi kanisa la Kuu St Patrick.

Viongozi wengine walishiriki Mazishi hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Katibu Mkuu wa UWT, Wabunge kutoka mkoa wa Morogoro na Mbunge wa jimbo la Korogwe Marry Chatanda, Wakuu wa Wilaya zote za mkoa huo, IGP mstaafu Mahita, Mwenyeviti wa Chama wa Wilaya zote wakiongoza kamati za siasa za Wilaya zao, wakuu wa vyombo vya ulinzi na ulinzi na Usalama mkoa huo, wakuu wa taasisi za umma pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

Mwendo Umeutimiza, Pumzika kwa Amani


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post