MKUCHIKA ATOA ONYO KWA WATUMISHI WA UMMA WANAOKAA NA BARUA ZA WATU BILA KUWAFIKISHIA WAHUSIKA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti, Utumishi wa Umma na Utawala bora Kepteni Mstaafu George Mkuchika amewakemea viongozi wa umma wanaokaa na barua za uhamisho wa watumishi bila kuwafikishia wahusika.

Mkuchika ameyasema hayo jijini Dodoma Disemba 6,2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu yatakayofanyika Disemba 11,2019 Jijini hapa.

Amesema kuna watu baadhi ya viongozi wanachukua nafasi ya Katibu Mkuu Utumishi kwa kukaa na barua za wafanyakazi wao kinyume cha sheria za utumishi wa umma.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hiyo wanapanga kufanya semina kwa viongozi na watumishi wa umma Kuhusu utawala bora na misingi ya maadili.

Mkurugenzi wa idara ya ukuzaji maadili katika Wizara ya Utumishi Fabiani Pokela amesema Serikali inataka taasisi wote ziweke mfumo wa ushughulikiaji wa malalamio ambayo yanatokea kwa wateja mbalimbali yanasababishwa na watumishi wa umma.

Siku ya maadili mwaka huu itafanyika Jijini Dodoma Disemba 11, 2019 ikiwa na kauli mbiu isemayo ‘kuwa maadili katika utumishi wa umma ni nguzo muhimu katika kuimarisha utawala bora na haki za binadamu’.

Mwisho.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post